Kauli ya Lissu yazidisha fukuto Chadema
Dar es Salaam. Katika hali inayoendelea kufukuta ndani ya Chadema, kufuatia kauli ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho (Bara), Tundu Lissu kwamba kuna fedha zimemwagwa katika uchaguzi wa ndani, kikao cha Kamati Kuu kinachosubiriwa ndio kinatajwa kutegua kitendawili. Kikao hicho ambacho hata hivyo tarehe yake haijapangwa, kinatarajiwa kuwa cha moto, huku hoja ya fedha kumwagwa…