Takukuru kujitosa madai ya rushwa uchaguzi ndani ya Chadema
Dar es Salaam. Taasisi Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imesema inafuatilia taarifa zozote za rushwa katika uchaguzi, zikiwemo zilizotolewa na Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu kuwa kuna fedha zimemwagwa kwenye uchaguzi wa ndani wa chama hicho. Lissu alitoa madai hayo jana Mei 2, 2024 alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara mjini Iringa, akihoji…