Blinken ziarani Israel kutafutia suluhu vita vya Gaza – DW – 01.05.2024
Blinken amekutana kwa mazungumzo na viongozi wa Israel na kusema “wakati ni sasa” wa kufikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano katika vita Gaza, huku akilitupia lawama kundi la Hamas kwa kucheleshwa kwa makubaliano hayo: ” Tumedhamiria kufikiwa kwa makubaliano ya usitishaji mapigano ambayo yatawarejesha nyumbani mateka. Tunatakiwa kufikia mpango huo sasa. Na sababu pekee ambayo hilo…