
Simbu, Gisemo kubeba mioyo ya Watanzania Tokyo
MATUMAINI ya Tanzania kuongeza medali ya tatu katika historia ya mashindano ya dunia ya riadha yapo mikononi mwa wanariadha wawili Aphonce Simbu na Josephat Gisemo watakaoshiriki kuanzia Septemba 13, mwaka huu, jijini Tokyo, Japan. Awali, Tanzania ilitarajia kupeperusha bendera kwa wanariadha wanne, lakini mipango hiyo ikayumba baada ya bingwa wa marathoni wa Wanawake, Magdalena Shauri…