WATANZANIA SABA WAWASILI NCHINI KUTOKEA IRAN
Watanzania SABA waliokuwa nchini Iran wamewasili jijini Dar es Salaam Machi 13, 2026, kufuatia operesheni ya uokozi iliyoratibiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Watanzania hao wamewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 8:40 usiku kwa kutumia Shirika la Ndege la Uturuki, wakitokea nchini Uturuki ambako walipokewa awali…