
Aliyekuwa Spika Bunge la Ukraine auawa kwa kupigwa risasi
Dar es Salaam. Aliyekuwa Spika wa Bunge la Ukraine, Andriy Parubiy ameuawa kwa kupigwa risasi katika Jiji la Magharibi la Lviv jana Jumamosi, kwa mujibu wa taarifa za Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu. Taarifa zinaeleza kuwa, mtu mwenye silaha alifyatua risasi kadhaa na kumuua Parubiy papo hapo kisha kukimbia na msako mkubwa umeanzishwa kumtafuta muuaji…