
Tanesco yaja na teknolojia ya matengenezo bila kukata umeme
Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), limefanya matengenezo kinga kwenye njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovoti 220 kutoka Kituo cha kupoza umeme Chalinze hadi Kituo cha Kinyerezi Dar es Salaam bila kuzima umeme (live line). Teknolojia hiyo ya ‘live line’ inalenga kupunguza upotevu wa umeme kutokana na kuzima laini pamoja na…