TBS YAWATAKA WAZALISHAJI WA MKAA MBADALA KUZINGATIA VIWANGO
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetoa mafunzo kwa wajasiriamali wanaozalisha nishati safi ya kupikia, hususan mkaa mbadala, mkoani Kigoma kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuzalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya viwango. Mafunzo hayo yamelenga kuwasaidia wazalishaji hao kuboresha ubora wa mkaa mbadala wanaozalisha ili uweze kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya Tanzania….