
Waliokuwa watumishi Kigamboni wapandishwa kizimbani
Dar es Salaam. Aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Fedha na Mhasibu wa Manispaa ya Kigamboni, Jonathan Manguli (38) na wenzake 12, wakiwamo wafanyabiashara wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashtaka 10, yakiwamo ya kuchepusha fedha na kuisababishia Wizara ya Tamisemi hasara ya Sh165 milioni. Washtakiwa wengine waliokuwa watumishi wa manispaa hiyo ni mhasibu Godfrey Martiny (44), mkuu…