
Abiria treni ya Ubungo walalamikia ubovu wa reli, giza usiku, kung’atwa na mbu
Dar es Salaam. Abiria wanaotumia treni ya Kariakoo kwenda Ubungo maarufu kama Treni ya Mwakyembe wamelalamikia ubovu wa kipande cha reli kutoka Barabara ya Mandela hadi Kwa Mnyamani, Buguruni, hali inayowafanya kurushwarushwa na kugongana wakati wa safari. Wakizungumza na Mwananchi Digital kwa nyakati tofauti, abiria hao wameiomba TRC kuitupia jicho reli hiyo kabla haijasababisha maafa….