Walimu hawana miujiza kumbadili mwanao
Dar es Salaam. Katika jamii nyingi za leo, imezuka dhana potofu kwamba kazi ya kulea watoto ni ya walimu. Wazazi wengi wamejikuta wakitelekeza jukumu lao la msingi, wakikabidhi watoto wao kwa walimu kana kwamba shule ndiyo nyumba ya pili ya mtoto kwa kila jambo. Mtoto anaposhindwa kimaadili au kielimu, lawama huelekezwa kwa walimu kwa haraka mno,…