
KONA YA MALOTO: No Reforms, No Election, Oktoba Tunatiki ni kipimo nchi inaumwa
Taifa limetekwa na mkumbo wa kauli mbiu (slogan). Upande mmoja ulianza kuchafua mitandao ya kijamii kwa kuandika maoni kwenye kila posti ya mtu maarufu; No Reforms, No Election. Kwamba bila mabadiliko ya sheria hakutakuwa na uchaguzi. No Reforms, No Election ni kauli mbiu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), msingi wake ni kusukuma presha…