
NIKWAMBIE MAMA: Huu mtego wa panya uliomnasa ng’ombe
Nikikumbuka stori ya mtego wa panya huwa napata woga sana. Katika stori hii, panya anauona mnofu wa samaki aliotegewa. Anamwomba jogoo autegue ili apate riziki yake, lakini pia anatahadharisha kuwa mtego wa panya una hatari kubwa. Haumchagui panya pekee bali hunasa waliomo na wasiokuwamo. Jogoo anampuuza na kwenda na hamsini zake. Panya anamwendea mbuzi, lakini…