
Hela ya mstaafu inapokopwa bila kurejeshwa!
Siku chache zilizopita, macho na masikio ya mstaafu wetu ambayo uzee wake sasa huyafanya yasione wala kusikia vizuri, pamoja na kupenda kwake kuyafagilia kuwa yameona na kusikia mengi yamemfanya kusoma na kusikia mengi. Mengi hayo ni yale yanayoishia kupandisha shinikizo lake la damu na kuharakisha safari yake ya kuelekea Kinondoni kwa kasi zaidi ya G6…