Dk Mwinyi kuchukua fomu Agosti 30, wasanii kunogesha

Unguja. Baada ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kutoa ratiba ya kuchukua na kurejesha fomu, mtiania urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Hussein Mwinyi anatarajia kuchukua fomu Agosti 30, 2025. Siku hiyo baada ya kuchukua fomu, Dk Mwinyi ambaye ndiye Rais wa Zanzibar anayemaliza awamu ya kwanza ya utawala wake, atazungumza na…

Read More

Chrome City Yapagawisha Hustlers Kariakoo na Manzese Kuelekea Uzinduzi Agosti 30, Tanganyika Packers – Kawe.

Mishemishe na harakati za Kariakoo na Manzese zilinoga kipekee kwa ‘vibe’ la aina yake jana baada ya timu ya Chrome City kuingia mtaani kuungana na mashujaa halisi wa uchumi wa mijini Tanzania – hustlers. Kuanzia waendesha bodaboda, mama lishe, wauzaji wa nguo, wauzaji wa vifaa vya umeme, mpaka wauza matunda – kampeni hii inawatambua na…

Read More

Dk Migiro Katibu Mkuu mpya CCM

Dar es Salaam. Wakati Chama cha Mapinduzi (CCM) kikiteua wagombea ubunge na uwakilishi watakaopeperusha bendera yake katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025, pia kimemteua Dk Asha-Rose Migiro kuwa katibu mkuu wake mpya. Uteuzi huo umetangazwa leo Agosti 23, 2025 na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, makao makuu ya CCM, jijini Dodoma ikiwa…

Read More

Sauti Jasiri ya Kizazi Kipya – Global Publishers

Katika mitaa yenye shamrashamra ya Jiji la Dar es Salaam na kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii yanayoendelea kushika kasi Afrika Mashariki, jina moja limekuwa gumzo—Kamshange. Akitambulika kwa utu wake usio na woga, ukweli wake usio na kificho, na mvuto wake wa kipekee kwenye vyombo vya habari, Kamshange amejiwekea nafasi kama mmoja…

Read More

Hekaya za malevi: Akili mnemba kizibo cha akili – 2

Dar es Salaam. Siwezi kubishana na umati unaodai kuwa akili mnemba ni maendeleo. Hoja yangu ni lugha inayotumika  tukisema “Maendeleo ni kutoka mahala na kwenda mahala pengine”, haimaanishi kwenda kinyumenyume ni maendeleo. Hivyo nakusudia kusema kuwa matumizi ya akili mnemba bado hayajaeleweka sawasawa miongoni mwa watumiaji wake. Wanaiweka mbele wakidhani kuwa ina silika za ufundishaji….

Read More

Mboni Masimba amrudisha jukwaani Bi Mwanahawa Ally 

Mkurugenzi wa Kampuni ya Chocolate Princess,Mboni Masimba, amemrudisha jukwaani mkongwe wa Taarabu nchini, Mwanahawa Ally aliyetangaza kustaafu kuimba mwaka jana. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mboni amesema,  anatarajia kufanya tamasha la mkesha wa muziki wa taarabu litakalohusisha wakali wasanii wa muziki huo nchini akiwemo Mwanahawa Ally, Agosti 28 kwenye Viwanja vya…

Read More

Hizi hapa fursa za kiuchumi za uchaguzi mkuu

Dar es Salaam. Ukiacha mbilinge za kisiasa, vijembe na vituko katika majukwaa ya kampeni kuelekea uchaguzi mkuu, tukio hilo limebeba pia fursa za kiuchumi na biashara kwa wananchi. Kwa mujibu wa wadau mbalimbali wa biashara, tukio la uchaguzi linapaswa kutazamwa kwa jicho mtambuka, kwani linabeba fursa za kiuchumi na kibiashara, ambazo zinaweza kuwakwamua watu. Kuchapisha…

Read More