Wanne wateuliwa mabalozi wa utalii Zanzibar, yumo raia wa Ujerumani
Unguja. Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale imewateua mabalozi wanne wa utalii, wakiwemo raia wa ndani na wa kigeni zikiwa ni juhudi za kukuza na kutangaza utalii wa Zanzibar. Miongoni mwa mabalozi hao ni Alois Inninger, raia wa Ujerumani, ambaye anatarajiwa kusaidia kuvutia watalii kutoka nchi mbalimbali za Ulaya. Wengine walioteuliwa ni Ruqaiya Karanja,…