
Mbowe asimulia Lissu, Lema na Heche walivyomuumiza Chadema
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ameelezea maumivu mbalimbali anayopitia ndani ya chama hicho, akisema hayamkatishi tamaa kwani ndio wito aliouchagua. Amesema kwa zaidi ya miaka ya 30 akiwa ndani ya chama na miaka 21 ya uenyekiti amepitia mengi, ikiwemo viongozi wenzake waandamizi kumshambulia kwa maneno aliyodai ni…