
Hekaya za Mlevi: Sasa imbeni “miskanka mishisha”…
Dar es Salaam. Waswahili waliposema “Pombe siyo maji” hawakukosea hata kidogo. Ilitokea siku moja tukitayarisha mazishi ya rafiki yetu aliyetutoka siku moja kabla. Tukaliandaa kaburi kwa jinsi ilivyotakiwa, lakini tukiwa njiani kurudi msibani tukakiona kivuli. Tukaona si vibaya tukapate moja mbili za kutoa uchovu pamoja na kupunguza makali ya msiba. Tulikuwa kadiri ya watu sita tukiongozana…