Hekaya za Mlevi: Wapinzani hoyahoya mpaka lini?
Dar es Salaam. Siku moja tulishuhudia mtanange wa soka wa kushangaza sana. Lilikuwa “Ndondo Cup” enzi hizo likipigwa mchangani. Wengine walicheza peku, na timu iliyopungukiwa na jezi ilicheza matumbo wazi. Siku hiyo timu ya kitaani iliyokuwa bingwa mtetezi ilicheza fainali dhidi ya mahasimu wao wakubwa. Walipokutana hawa ilikuwa kama Simba na Yanga, kitaa kizima kilinuka….