
Rayvanny aibua shangwe ufunguzi CHAN 2024
DAKIKA chache kabla ya mchezo wa ufunguzi kati ya wenyeji Tanzania dhidi ya Burkina Faso uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rayvanny ameibua shangwe kwa mashabiki. Staa huyo ameingia uwanjani kutumbuiza katika sherehe za ufunguzi wa michuano hiyo akiimba wimbo wa Kitu Kizito aliomshirikisha Misso Misondo na kuibua vaibu kubwa…