
AKILI ZA KIJIWENI: Somo lingine tunalipata kwa Dulla Makabila
NDUGU yetu Dulla Makabila amekosa kirahisi fursa ya kupiga shoo kwenye kilele cha tamasha la Simba Day, keshokutwa Jumamosi. Kilichomponza ni mdomo wake mwenyewe ambao siku moja ulitoa maneno yasiyo na staha kwa Simba muda mfupi baada ya kutangaza amehamia Yanga. Jamaa baada ya kipindi fulani kutangaza kuhamia Yanga, aliibeza Simba kwa maneno mengi ya…