Seine-sational! Paris yatoa kwaheri ya ushindi kwa Olimpiki – DW – 12.08.2024
Cruise aliteremka kwenye waya mbele ya watazamaji 71,500, akashika bendera ya olimpiki na kurukia pikipiki, tukio lililowachangamsha wanariadha na mashabiki waliofurika katika uwanja wa Stade de France. Katika dondoo ya kile ambacho ulimwengu unaweza kutarajia wakati Michezo hiyo itakapoelekea Los Angeles mnamo 2028, nyota huyo wa “Mission Impossible” kisha alionyeshwa akipanda ndege na kuruka angani…