Aliyemuua shangazi yake akimtuhumu kwa uchawi, kunyongwa
Arusha. Mahakama ya Rufani imebariki adhabu ya kunyongwa hadi kufa aliyohukumiwa Sami Kisenga baada ya kukutwa na hatia ya kumuua shangazi yake, Holo Kisenga (50) kwa kumkata na panga kichwani na shingoni, akimtuhumu kuwa ni mchawi na amemuua baba yake. Mauaji hayo yalidaiwa kutokea Mei 19, 2019 katika Kijiji cha Nyaligongo, Mkoa wa Shinyanga. Sami…