Watanzania 236 waliokwama Dubai warejea nchini, wasimulia waliyopitia
Dar es Salaam. “Nilikuwa naomba Mungu kila siku nimwone tena mwanangu akiwa hai. Leo nimemkumbatia tena hapa uwanja wa ndege, siwezi kueleza furaha niliyonayo.” Hayo ni maneno ya mama aliyejitambulisha kwa jina moja la Sharifa, ambaye ameshindwa kuyazuia machozi ya furaha yaliyomtoka alipompokea mwanaye katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini…