Sauti iliyopazwa ziara ya Mwigulu yaleta mageuzi sekta ya elimu
Tanga. Mwaka 2007 wakati Kitongoji cha Chang’ombe, kilichopo Kijiji cha Mkata Magharibi, wilayani Handeni, Tanga kikiwa kinapambana kujenga misingi ya huduma za kijamii, ndoto ya kuwa na shule ya kisasa ilizaliwa. Kwa msaada wa Shirika la World Vision, Shule ya Msingi Imani ikajengwa mita 300 kutoka barabara kuu inayounganisha mikoa ya Kaskazini na nchi jirani….