Kihongosi aonya viongozi wanaodhulumu wananchi

Itilima. Mwananchi wa Kijiji cha Lagangabilili wilayani Itilima, mkoani Simiyu, Mzee Majija Madata amewasilisha malalamiko kwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi, akidai kudhulumiwa shamba lake na mmoja wa viongozi wa CCM katika ngazi ya wilaya mkoani Shinyanga. Kihongosi yupo mkoani Simiyu tangu Machi 7, 2026 kwa ziara…

Read More

DTB yawapongeza wafanyakazi wanawake kwa mchango wao

Dar es Salaam. Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani 2026 yenye kauli mbiu ya “Give to Gain”, Diamond Trust Bank Tanzania (DTB) imetoa zawadi maalum kwa wafanyakazi wake wanawake kama ishara ya kutambua mchango wao muhimu katika mafanikio ya taasisi hiyo ya kifedha. Hatua hiyo inalenga kuhamasisha usawa wa kijinsia na kuendelea kujenga mazingira jumuishi…

Read More

Huyu ndiye Mojtaba Khamenei, Kiongozi mpya wa Iran

Dar es Salaam. Kifo cha kiongozi mkuu wa Iran, Ali Khamenei, kilichotokea Februari 28, 2026, wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, kinaashiria moja ya mabadiliko makubwa zaidi katika historia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Mrithi wake, mwanaye, Mojtaba Khamenei, anawakilisha kwa wakati mmoja mwendelezo na pia mkanganyiko ndani ya mfumo wa mapinduzi ulioanzishwa baada…

Read More

Wabunge Chato, madiwani wanne wafikishwa kortini tuhuma za rushwa

Chato. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mkoa wa Geita imewafikisha mahakamani wabunge wawili wa Chato, Pascal Lutandula (Chato Kusini), Cornel Magembe wa (Chato Kaskazini) na madiwani wanne akiwemo aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chato, Bathoromeo Manunga wakituhumiwa kwa rushwa wakati wa mchakato wa kumpata mwenyekiti wa halmashauri hiyo. Mbali nao, wengine ni…

Read More

Shule Ya Msingi Kiromo Yakarabatiwa Kwa Ufadhili Wa Airtel

Bakari Mahundu March 9, 2026 0 Comments Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Charles Kamoto, ametembelea Shule ya Msingi Kiromo kukagua maendeleo ya mradi wa ukarabati unaofadhiliwa na kampuni hiyo, wenye lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi na walimu. Katika ziara hiyo, viongozi wa Airtel walipata taarifa ya hatua za ukarabati wa miundombinu ya…

Read More