OMO aahidi kurasimisha mazao ya bahari Zanzibar
Unguja. Mgombea wa Zanzibar kwa tiketi ya ACT – Wazalendo, Othman Masoud Othman, maarufu OMO, ameahidi kuyageuza mazao ya bahari kuwa sekta rasmi yenye mchango mkubwa ili kukuza uchumi wa visiwa hivyo. Othman ameeleza hayo leo Jumapili, Septemba 28, 2025 wakati akizungumza na wavuvi na waanikaji wa dagaa eneo la Mangapwani, Wilaya ya Kaskazini B,…