Wanafunzi NM-AIST wabuni roboti la ukaguzi viwandani
Arusha. Wanafunzi watatu kutoka Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela (NM-AIST), wamebuni roboti lenye uwezo wa kukagua chupa za vinywaji katika mchakato wa uzalishaji viwandani. Mashine hiyo iliyotengenezwa kwa ushirikiano wa Profesa Anaeli Sam, Dk Judith Leo na Jared Nganyi, inafanya kazi kwa mfumo wa kunyanyua na kushusha, ikiwa na mkono wa roboti…