CCM yaahidi uwanja wa ndege wa kimataifa Tanga

Tanga. Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema moja ya ahadi kubwa za chama hicho katika ilani ya uchaguzi 2025-2030 ni kujenga upya uwanja wa ndege wa Tanga na kuufanya wa kisasa wenye hadhi ya kimataifa. Akizungumza leo Jumatano Septemba 24, 2025 baada ya kuwasili jijini Tanga, Wasira amesema uwanja huo ulikuwa na…

Read More

Sababu Ramaphosa kuzimiwa kipaza sauti akihutubia UN

New York. Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amezimiwa kipaza sauti kwenye mkutano maalumu wa kujadili umuhimu wa kuanzishwa taifa huru la Palestina, baada ya kuelekeza mashambulizi dhidi ya Israel akidai inachofanya Gaza ni mauaji ya kimbari. Pia, alifananisha mateso ya Wapalestina wanayofanyiwa na Israel na waliyoyapata Waafrika Kusini wakati wa utawala wa ubaguzi wa…

Read More

Hamad: Wananchi wanahitaji chakula zaidi na si Katiba

Unguja. Mgombea urais wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Hamad Rashid Mohamed amesema chama chake kinahitaji kuwaendeleza wananchi kwa kuhakikisha wanapata chakula cha kutosha kwanza ili wawe na nguvu za kushiriki shughuli za uzalishaji na utafiti wa rasilimali za nchi, na si Katiba mpya. Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano, Septemba 24,…

Read More

Samia aomba kura Ruangwa akimtaja Majaliwa bado yupo

Ruangwa. Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan ameahidi kuendelea kumtumia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kama msaidizi muhimu kwenye Serikali yake pindi atakapochaguliwa kuwa madarakani. Majaliwa ambaye amekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa miaka 15 na kushika nafasi ya Waziri Mkuu kwa miaka 10,…

Read More

Washiriki wa Buildexpo Tanzania 2025 waitwa kujenga viwanda nchini

Dar es Salaam. Kampuni na taasisi mbalimbali zinazoshiriki katika maonesho ya biashara ya ujenzi, Afrika Mashariki yajulikanayo kama Buildexpo Tanzania 2025, zimetakiwa kuwekeza nchini kwa kuanzisha viwanda badala ya kuishia kushiriki maonyesho na kuzalisha bidhaa katika mataifa mengine. Wito huo umetolewa leo Jumatano Septemba 24, 2025 na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Janeth Lekashingo wakati…

Read More

Askofu Munga azikwa, jamii ikiaswa juu ya upendo

Mkinga. Mazishi ya Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dk Stephen Munga, yametawaliwa na nasaha za kuwaasa Watanzania kuimarisha amani na upendo, badala ya kujenga chuki. Dk Munga amezikwa leo, Septemba 24, 2025, saa 9:30 alasiri ndani ya kanisa lililopo Kijiji cha Maramba, wilayani Mkinga, mkoani Tanga….

Read More

Serikali yatoa kauli  mradi wa Liganga, Mchuchuma

Dar es Salaam. Baada ya changamoto zilizodumu kwa muda mrefu, Serikali ya Tanzania imesema mazungumzo kuhusu mradi wa chuma wa Liganga na makaa ya mawe wa Mchuchuma yamefikia hatua ya uamuzi, huku hoja zilizokuwa zikisababisha ucheleweshaji kama mgawanyo usio sawa wa hisa na masharti ya mikataba yaliyowapendelea zaidi wawekezaji wa kigeni zikishughulikiwa. Akizungumza leo Jumatano,…

Read More