Sh3 milioni zamweka matatani Mtendaji wa kijiji Simanjiro
Simanjiro. Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Ruvu Remit wilayani Simanjiro mkoani Manyara, Godbles Mollel amefikishwa mahakamani kwa kosa la rushwa kwa kutumia Sh3.3 milioni isivyo halali. Mollel amesomewa shitaka hilo la uhujumu uchumi leo Septemba 17, 2025 mbele ya hakimu mkazi mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, Onesimo Nicodemo. Mwendesha mashtaka wa…