Wasira: CCM tulifanya uamuzi sahihi kwa Samia

Makete. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema uamuzi wa kumchagua Samia Suluhu Hassan awanie kiti cha urais kupitia CCM siyo kumpa zawadi bali ni kutokana na uwezo aliouonesha kuiongoza nchi kwa mafanikio makubwa. Kimesema Samia licha ya kuichukua nchi katika mazingira magumu, lakini aliivusha salama na maendeleo makubwa yameshuhudiwa chini ya uongozi wake. Miongoni mwa mafanikio…

Read More

Sekondari ya Temeke yapigwa tafu vifaa vya maabara

Dar es Salaam. Katika kutekeleza mkakati wa kuinua ubora wa elimu ya sayansi nchini Tanzania, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa msaada wa Sh10 milioni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya maabara katika Shule ya Sekondari Temeke. Fedha hizo zimekabidhiwa shuleni hapo, kwa ajili ya kununua vifaa vya maabara…

Read More

Othman awaahidi wavuvi Zanzibar mikopo, zana za kisasa

Pemba. Mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha ACT- Wazalendo, Othman Masoud Othman, ameahidi kufanya mageuzi katika sekta ya uvuvi ikiwemo kuboresha miundombinu ya bandari na masoko ya samaki ili kuongeza kipato cha wavuvi. Othman amefafanua kuwa maboresho hayo yatawezesha wavuvi kupata sehemu nzuri za kuhifadhia mazao yao ili kufanya shughuli zao kwa ufanisi zaidi….

Read More

Huduma jumuishi za kifedha zaipa BoT tuzo ya kimataifa

Dar es Salaam. Utekelezaji wa matumizi ya mfumo wa malipo ya papo kwa papo (TIPS) na matumizi ya msimbo namba (QR code) unaofahamika kama TANQR, umetajwa kuwa sababu ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kutunukiwa tuzo kuu ya ubunifu katika huduma jumuishi za fedha. Tuzo hiyo ijulikanayo kama Nestor Espenilla Jr. Financial Inclusion Innovation Award,…

Read More

Lissu aibua jipya kuhusu mashahidi wa Jamhuri

‎Dar es Salaam.  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, ameibua hoja mpya dhidi ya mashahidi wa Jamhuri wanaotarajiwa kutoa ushahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili, akidai kuwa ni hawastahili kisheria kufika mahakamani kutoa ushahidi kwenye kesi hiyo. Lissu ameibua madai hayo leo Jumanne, Septemba 16, 2025, katika mwendelezo wa usikilizwaji wa…

Read More

Usimamizi mbovu mikataba ya miradi ya ujenzi unavyoigharimu Serikali mabilioni ya fedha

Arusha. Usimamizi mbovu wa mikataba ya miradi ya ujenzi wa miundombinu ya usafiri imetajwa kama kaa la moto, linaloteketeza mabilioni ya fedha za Serikali. Kutokana na hilo, Serikali imewataka wataalamu wa sekta ya ujenzi na usafirishaji kuhakikisha wanaongeza uelewa, umakini na kuweka uwazi katika mikataba ya miradi ya miundombinu, ili kulinda thamani ya fedha za…

Read More