Mavunde aonya wakopaji dhidi ya mikopo umiza
Dodoma. Mgombea ubunge wa Mtumba, Anthony Mavunde amesema kukopa bila elimu ya ujasiriamali na fedha ni chanzo cha mikopo umiza. Kutokana na hilo, amewataka wananchi hasa kinamama na vijana kuacha kukopa kwa kuiga kwani watajikuta wameingia mahali penye hasara kubwa. Mavunde ametoa kauli hiyo jana Jumamosi Septemba 13,2025 kwa nyakati tofauti alipokuwa kwenye ziara ya…