Mambo 11 yaliyoibeba sekta ya utalii dhidi ya Uviko-19

Dar es Salaam. Wakati sekta ya utalii duniani ikirejea katika nafasi iliyokuwapo kabla ya ugonjwa wa Virusi vya Korona (Uviko-19), haya hapa mambo 11 yaliyoibeba sekta hii kwa Tanzania. Mambo hayo kwa mujibu wa Ripoti yamechangia kuongezeka kwa mapato ya utalii nchini kwa asilimia 15.7 hadi kufikia dola za Kimarekani bilioni 3.903 (Sh10.15 trilioni) mwaka…

Read More

Ripoti Mpya ya Elimu Yaangazia Uhitaji wa Kutumia Utafiti kwa Sera Elekezi Kukabiliana na Umaskini wa Kujifunza Ulimwenguni

Ijumaa, 5 Septemba 2025 – Embu, Kenya. Ripoti mpya ya elimu imetoa wito kuchukua hatua za haraka kulingana na ushahidi wa kitafiti ili kushughulikia mapungufu yaliyopo, hayo yameangaziwa katika Mkutano wa Sita wa Education Evidence for Action (EE4A) na EDF unaofanyika kila baada ya miaka miwili kabla ya kuzinduliwa rasmi baadaye mwaka huu. Ripoti hiyo inapendekeza tafsiri ya haraka ya…

Read More

NMB Yakabidhi Jezi za Milioni 36 kwa Shimiwi

Benki ya NMB imekabidhi jezi zenye thamani ya Shilingi milioni 36 kwa Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (Shimiwi), ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za kukuza michezo miongoni mwa watumishi wa umma nchini. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi wa Shimiwi wakiongozwa na…

Read More

Msajili, CAG waguswa kesi ya rasilimali Chadema

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekana kuwa na nyaraka kuhusu rasilimali zake zilizoombwa katika kesi ya mgogoro wa mgawanyo wa rasilimali inayokikabili. Kimesema Msajili wa Vyama vya Siasa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ndio wenye baadhi ya nyaraka zinazoombwa. ‎Kesi hiyo ya madai namba 8323 ya…

Read More

Mgombea urais UDP aahidi majisafi, elimu bure hadi chuo kikuu

Geita. Mgombea urais wa Chama cha United Democratic Party (UDP),  Saumu Rashid amesema chama chake kimejipanga kutatua changamoto kubwa zinazowakabili Watanzania kwa kuhakikisha upatikanaji wa majisafi na salama, elimu bure hadi chuo kikuu, huduma za afya nafuu na uwekezaji wenye tija katika rasilimali za Taifa. Akizungumza leo Septemba 10, 2025 kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika…

Read More

Nyuki walioweka makazi Msamvu watimka na kung’ata watu

Morogoro. Baadhi ya watumiaji wa vyombo vya moto, baiskeli na watembea kwa miguu wameng’atwa na nyuki waliokuwa wamevamia eneo la Msamvu Mataa, Manispaa ya Morogoro, huku wengine wakipata majeraha baada ya kudondoka na vyombo vyao vya usafiri wakijaribu kuwakimbia nyuki hao. Tukio hilo limetokea leo Jumatano Septemba 10 kwenye nguzo za taa za barabarani zilizopo…

Read More