TPA yaja na mkakati wa soko la DRC

Dar es Salaam. Baada ya mkakati wa maboresho kuongeza ufanisi wa utendaji wake, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) sasa imegeukia kuyasaka masoko, ikianza na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). DRC inachangia zaidi ya asilimia 40 ya mizigo yote inayosafirishwa kupitia Bandari ya Dar es Salaam, kwa mujibu wa ripoti ya TPA ya…

Read More

Wachambuzi wataja sababu Tanzania kupaa maboresho ya utawala bora kidunia

Dar es Salaam. Wachambuzi wa masuala ya uongozi na utawala bora nchini wamesema mageuzi ya falsafa ya utawala yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kutatua changamoto zilizokuwapo awamu ya tano, yamechangia kupanda viwango kwenye kipimo cha utawala bora duniani. Kauli hiyo inakuja kufuatia ripoti ya Chandler Good Government Index (CGGI) 2025, iliyoonesha kuwa, Tanzania…

Read More

Mpango wa afya kwa wote waanza, 3,561 wakihitimu

Lindi. Safari ya kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma za afya bila vikwazo vya kiuchumi imeanza rasmi, baada ya wahudumu wa afya ngazi ya jamii 3,561, kati ya 137,294 wanaotarajiwa nchi nzima, kuanza kutoa huduma baada ya kupatiwa mafunzo na vitendea kazi. Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Grace Magembe, amesema hayo leo, Jumatatu, Septemba 8, 2025,…

Read More

Makamba alivyowaaga Bumbuli, amnadi Samia na mgombea ubunge

Tanga. Ni furaha na huzuni vilitawala wakati aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga, January Makamba aliposimama kwenye jukwaa kuwaafa wananchi hao baada ya kuwatumikia kwa miaka 15. Huzuni na furaha hiyop ulitokana na baadhi ya wananchi kueleza jinsi wanavyokumbuka nyakati za shida na raha wakati Makamba alipokuwa akiwatumikia ndani ya miaka hiyo. Pamoja…

Read More

Kifo cha fundi ujenzi chazua utata Mirerani

Mirerani. Fundi ujenzi wa nyumba Mtaa wa Msikiti, Mji Mdogo wa Mirerani, wilayani Simanjiro, mkoani Manyara, Salimu Kijuu (42) amefariki dunia huku kifo chake kikidaiwa kuwa na utata, baada ya mwili wake kukaa ndani kwa zaidi ya siku tatu bila kujulikana. Mwili wa marehemu umegundulika Septemba 7,  2025 saa 7 mchana baada ya eneo alilokuwa…

Read More

Lissu aibua mapya kesi yake ya uhaini

Dar es Salaam. Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, imeshindwa kuendelea kusikilizwa katika hatua ya awali kama ilivyokuwa imepangwa. Hali hiyo imesababishwa na mambo mapya yaliyojitokeza, ikiwamo suala la jopo la majaji na Lissu kumkataa wakili aliyeteuliwa na Mahakama kumwakilisha. Katika kesi hiyo, Lissu anakabiliwa na shtaka…

Read More