Jaji Mkuu awaondolea mapumziko majaji, mahakimu Zanzibar

Unguja. Kutokana na mchakato wa wagombea urais na uwakilishi kutakiwa kula viapo mahakamani, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Khamis Ramadhan Abdalla ameagiza watendaji wote wa mahakama kuwa kazini hata siku za sikukuu na mapumziko ya mwishoni mwa juma. Hatua hiyo inalenga kuwapatia fursa wagombea wanaosaka nafasi hizo kufika mahakamani kula viapo mbele ya majaji na mahakimu….

Read More

Nafasi ya huduma rasmi za kifedha katika Dira 2050

Dar es Salaam. Wananchi wametakiwa kutumia mifumo rasmi ya kifedha ikiwemo huduma za benki ili kuiwezesha Tanzania kutimiza malengo ya kuwa taifa lenye uchumi jumuishi na shindani ifikapo 2050. Hayo yalielezwa jana Septemba 04, 2025 wakati wa kongamano lililoandaliwa na Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) likilenga kuangazia fursa na changamoto za sekta hiyo katika utoaji…

Read More

NI NYOMI TU KILA ANAKOKWENDA MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DK.SAMIA SULUHU HASSAN

*Aacha matumaini makubwa kwa wakulima wa zao la parachichi ,Chai wilayani Rungwe  *Mashamba ambayo wawekezaji wameshindwa kuyaendeleza Serikali yaunda timu kufuatilia Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Rungwe KAMPENI za mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk.Samia Suhusu Hassan zimeendelea katika Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya ambapo maelfu ya wananchi wamejitokeza kwenye mkutano huo. Akiwa katika…

Read More

Dk Mwinyi awapa jukumu viongozi wa dini ulinzi wa amani

Unguja. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi, amewataka viongozi wa dini kutumia majukwaa yao kupaza sauti na kuwakumbusha wanasiasa kuwa katika kipindi cha kampeni ni muhimu kuepuka siasa za chuki, mifarakano, ubaguzi na matusi. Amesema badala ya kueneza maneno ya uchochezi, wanasiasa wanapaswa kueleza kwa uwazi mipango na sera zao kuhusu namna watakavyowahudumia wananchi,…

Read More

Ebola yaibuka tena DRC, yaua watu 16

Kinshasa. Mamlaka za afya za Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zimetangaza mlipuo mpya wa ugonjwa wa Ebola, ambapo hadi sasa umeua watu 16, wakiwepo wahudumu wanne wa afya. Pia zimeeleza kuwa hadi sasa watu 28 wameripotiwa kuambukizwa ugonjwa huo na baadhi yao wanaendelea na matibabu. Maeneo yaliyoathirika zaidi na mlipoko wa ugonjwa huo yanatajwa…

Read More

MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT.SAMIA SULUHU HASSAN AWAJIBU WANAOSEMA CCM INABEBA WATU NA MAGARI KUJAZA UWANJA

Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Rungwe MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk.Samia Suluhu Hasan amewajibu wanaosema Chama hicho kinabeba wanachama wake kwenye magari kuwapeleka katıka mikutano ya kampeni zake ambapo amesema siyo shida wala siyo aibu kuwasafirisha wanaokwenda katika mikutano. Akizungumza mbele ya maelfu ya wananchi wa Wilaya Rungwe mkoani Mbeya wakati wa mkutano…

Read More

Chaja (USB) zinavyogeuka mawindo ya wadukuzi

Shinyanga. Bila shaka umewahi kusikia kuhusu udukuzi mtandao ambao mara nyingi umekuwa ikihusishwa na mifumo ya intaneti kufika data ambazo mwenyewe hakutaka zifikiwe na mtu mwingine. Na pengine utakuwa umesikia kuhusu hatari ya kutumia WiFi za bure ambazo hazina ulinzi (unencrypted WiFi) na namna zinavyogeuka kuwa mawindo ya wadukuzi wenye nia tofauti. Ukiachana na hiyo,…

Read More