
Haya hapa maeneo hatari kwa ajali Mbeya, Tanroad yataja mwarobaini
Mbeya. Ajali za barabarani zinazotokea mara kwa mara mkoani Mbeya zimeendelea kugharimu maisha ya watu kutokana na maeneo korofi ambayo yakifanyiwa kazi huenda yakapunguza au kumaliza changamoto hiyo. Katika siku za hivi karibuni, kumekuwapo na ajali kadhaa zilizotokea mkoani hapa na kusababisha vifo na majeruhi, ikiwamo iliyotokea jana Juni 5, 2024 kwenye mteremko wa Simike…