
Wafuasi wa chama cha siasa BSW Ujerumani waipinga AFD – DW – 04.06.2024
Wachambuzi wanasema chama cha siasa za mrengo mkali wa kulia cha AfD ndicho kinapaswa kuwa na wasiwasi mkubwa kutokana na chama hiki kipya kinachojulikana kwa kifupi kama BSW. Wakati mwanasiasa mashuhuri wa mrengo wa kushoto Sahra Wagenknecht alipotangaza kuwa anaanzisha chama chake mwaka jana, baadhi walikitaja chama hicho kuwa mbadala kwa chama cha siasa kali…