
Ukarabati kivuko cha MV Magogoni kukamilika Desemba
Dodoma. Bunge limeelezwa ukarabati wa kivuko cha Mv Magogoni utakamilika mwishoni mwa Desemba, 2024 na kitaanza kutumika. Naibu Waziri wa Ujenzi, Godfrey Kasekenya amesema hayo leo Alhamisi, Mei 30, 2024 akijibu swali la msingi la mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile. Mbunge huyo alihoji ni lini matengenezo ya Mv Magogoni nje ya nchi yatakamilika na…