Wafungwa wapiga kura Afrika Kusini

Afrika Kusini. Wakati wananchi wa Afrika Kusini wakipiga kura leo Mei 29, 2024, wafungwa katika gereza la Pollsmoor la Cape Town nao wamepiga kura kwa mujibu wa taarifa za serikali. Chini ya Kifungu cha 24B cha Sheria ya Uchaguzi, wafungwa nchini Afrika Kusini wanaruhusiwa kupiga kura katika wilaya wanazoshikiliwa. Gereza la Pollsmoor lina umuhimu wa…

Read More

Ujenzi Daraja la Jangwani wanukia

Dodoma. Serikali imesema katika mwaka wa fedha wa 2024/25 itaanza utekelezaji wa mradi wa kimkakati wa ujenzi wa Daraja la Jangwani. Ujenzi huo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa maendelezo ya Bonde la Mto Msimbazi. Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema hayo bungeni leo Jumatano Mei 29 2024  alipowasilisha makadirio ya mapato na…

Read More

TGNP YAWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WA HABARI

Na Mwandishi wetu MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP), umetoa mafunzo kwa waandishi wa habari 24 kutoka vyombo vya habari ngazi ya kijamii ambayo yamelenga kuongeza uelewa na uwezo kwa waandishi hao ili waweze kutambua nafasi zao katika jamii. Akifungua mafunzo hayo ya siku tatu yanayofanyika Makao makuu ya TGNP Mtandao jijini Dar es salaam Leo…

Read More

Rais Samia kufanya ziara ya siku 7 Korea Kusini

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku saba, Jamhuri ya Korea, kufuatia mwaliko wa Rais wa nchi hiyo Yoon Suk Yeol. Ziara hiyo itaanza tarehe 31 Mei hadi 6 Juni 2024. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea). Akiwa nchini humo, Rais Samia atafanya mazungumzo rasmi Ikulu…

Read More

Sugu ambwaga Msigwa uenyekiti Chadema Kanda ya Nyasa

Njombe. Aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Mjini,  Joseph Mbilinyi, maarufu Sugu ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Nyasa akimbwaga mpinzani wake Mchungaji Peter Msigwa. Sugu amemshinda Msigwa ambaye alikuwa anatetea nafasi yake kwa kura 54 kwa 52 na sasa kada huyo ataiongoza kanda hiyo kwa miaka mitano…

Read More

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA KALI VISHOKA WANAOSHIKILIA MAENEO YENYE MALIGHAFI ZA UJENZI

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali wale wote watakaobainika kujihusisha na mchezo mchafu wa kushikilia maeneo yenye malighafi za ujenzi. Bashungwa ameyasema hayo wakati wa kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/25, Bungeni jijini Dodoma leo, Mei 29, 2024 Amesema changamoto kubwa ni uwepo wa vishoka wanaoshikilia maeneo…

Read More

Chuo cha KAM chaanza kudahili wanaosomea kozi za afya

CHUO cha Afya cha KAM College kilichopo Kimara jijini Dar es salaam ambacho kimebobea kwenye mafunzo ya sekta ya afya, kimepongeza juhudi za serikali katika kuwekeza kwenye miundombinu bora ya sekta ya afya. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea). Pongezi hizo zimetolewa leo Jumatano na Mkurugenzi wa Chuo hicho, Dk. Kandore Musika wakati akizungumza kuhusu  Baraza la…

Read More

‘Energy drinks’ zaibua mjadala Baraza la Wawakilishi

Unguja. Sakata la madhara yanayosababishwa na vinywaji vya kuongeza nguvu (energy drinks) limeibukia katika Baraza la Wawakilishi, ikielezwa kuna utafiti unaonyesha kinywaji hicho ni hatari kwa afya ya binadamu. Katika swali la msingi leo Mei 29, 2024, mwakilishi wa Wingwi, Kombo Mwinyi Shehe ametaka kujua ni kwa kiwango gani Serikali inafahamu tatizo hilo akieleza kuna…

Read More