
Spika aunda kamati kuchunguza mgogoro shamba la Ephata Malonje
Dodoma. Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackson ameunda kamati maalumu ya Bunge ya kuchunguza mgogoro kati ya wawekezaji wa shamba la Efatha la Malonje mkoani Rukwa na wanakijiji wanaolizunguka shamba hilo. Dk Tulia ametoa uamuzi wake leo Jumatatu, Mei 27, 2024 katika taarifa yake aliyoisoma muda mfupi kabla ya kuahirisha shughuli za Bunge,…