
MATARAJIO YA SERIKALI NI KUONA UZALISHAJI KATIKA KIWANDA CHA SUKARI MTIBWA UNAREJEA KWA HARAKA: WAZIRI NDEJEMBI
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MVOMERO WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Deogratius Ndejembi, amesema ni matarajio ya Serikali kuona uzalishaji katika kiwanda cha sukari cha Mtibwa unarejea kwa haraka. Mhe. Ndejembi ametoa kauli hiyo hivi karibuni alipofika katika kiwanda hicho ili kujionea mwenyewe hali halisi iliyopelekea ajali…