Askofu Shoo: Chagueni viongozi wenye hofu ya Mungu

Mtwara. Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Fredrick Shoo amewataka Watanzania kuwakataa viongozi wabinafsi hasa wanaowatelekeza wapigakura baada ya kushinda uchaguzi. Akizungumza kwenye ibada ya kitaifa katika kilele cha maadhimisho ya siku ya CCT iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) mjini Mtwara jana Mei 26, 2024, Askofu Shoo amesema kuwa…

Read More

MTINDO BORA WA MAISHA KINGA YA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

Na WAF – Geneva, Uswisi Imeelezwa kuwa uzingatiaji mtindo bora wa maisha ikiwemo kufanya mazoezi pamoja na ulaji wa vyakula unaofaa kwa kupunguza matumizi ya chumvi, sukari na mafuta husaidia kupunguza magonjwa Yasiyoambukiza. Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo leo Mei 27, 2024 baada ya matembezi maalum yajulikanayo kama ‘Walk the Talk, the…

Read More

Wafanyabiashara toeni ushirikiano wakutosha kwa timu ya uelimishaji kutoka TRA

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Batilda Buriani amewataka wafanyabiashara kutoa ushirikiano wa kutosha kwa timu ya uelimishaji kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambayo inaendelea kutoa elimu ya kodi mlango kwa mlango kwa wafanyabiashara kwa kuwatembelea katika maeneo yao ya biashara. Amewaomba wafanyabiashara wafunguke kwa TRA ili waweze kusikilizwa na kutatuliwa changamoto zao za…

Read More

Watu saba wafariki dunia mtumbwi ukipinduka Katavi

Katavi. Watu saba wamefariki dunia baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kupasuka kisha kupinduka Halmashauri ya Mlele, Kitongoji cha Lungunya mkoani Katavi. Vifo hivyo vimetokea hii jana Jumapili, Mei 26, 2024 ambapo inaelezwa mtumbwi ulikuwa umebeba watu 14 na magunia 10 ya mpunga hivyo ukashindwa kuhimili uzito huo. Hadi usiku wa jana ni mwili mmoja umepatikana…

Read More

CCM YAZINDUA KAMPENI UCHAGUZI MDOGO KWAHANI Z’BAR.

 NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR.   NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa, amewasihi Wananchi wa Jimbo la Kwahani kufanya maamuzi sahihi ya kumchagua mgombea aliyesimamishwa na CCM kwani ndiye mwenye uwezo wa kuendeleza utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 kwa vitendo.   Nasaha hizo amezitoa wakati akizindua kampeni za…

Read More

Fedha zadaiwa chanzo danadana mradi SGR

Dar es Salaam. Hofu  ya kukamilika kwa mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) inaendelea kupata mashiko, kufuatia kuendelea kushuhudiwa kwa ahadi zisizotimizwa za kukamilishwa utekelezwaji wa vipande mbalimbali vya ujenzi huo. Sambamba na ahadi zisizotimizwa, Mwananchi imeshuhudia wafanyakazi katika kambi mbalimbali wakiondolewa na mkandarasi kwa kile kinachodaiwa kuwa  Serikali haina fedha ya kumlipa kuendelea na…

Read More

Lissu: Ugumu wa maisha utamalizika tukipata Katiba mpya

Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)-Bara, Tundu Lisu amesema suluhisho la kumaliza ugumu wa maisha uliotamalaki nchini Tanzania ni kwa wananchi wakubali kuanza kutafuta Katiba Mpya. Amesema ugumu huo unachangiwa na upungufu wa Katiba iliyopo kiasi kwamba imezalisha utawala wa viongozi wenye miungu wengi wanaopanga maisha ya watu badala…

Read More