
DC Kaganda aagiza wafanyabiashara Ngaramtoni kufungiwa maduka yao
Arusha. Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Emmanuela Kaganda amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha DC kuwafungia maduka wafanyabiashara wa eneo la Ngaramtoni hadi watakapofanya usafi kwenye mitaro iliyo karibu na maduka yao. Mbali na hilo, amemtaka pia mkurugenzi huyo kuwapiga faini wafanyabiashara wote wa eneo hilo kwa mujibu wa sheria ya utunzaji wa mazingira, kwa…