Kesi ya mtoto wa Askofu Sepeku dhidi ya Kanisa la Anglikana kuunguruma tena leo
Dar es Salaam. Kesi ya Bernardo Sepeku ambaye ni mtoto wa marehemu John Sepeku aliyekuwa Askofu wa kwanza wa Kanisa Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Dar es Salaam, inaendelea leo Ijumaa, Agosti 29, 2025 Mahakama Kuu, Divisheni ya Ardhi. Bernardo amefungua kesi mahakamani hapo, akipinga kunyang’anywa zawadi ya kiwanja alichopewa baba yake mwaka 1978 na kanisa…