Vijana 2,000 kujadili ajenda, nafasi za uchaguzi 2024/25  

Dodoma. Zaidi ya vijana 2,000 kutoka vyama vya siasa, asasi za kiraia na Serikali wanatarajiwa kushiriki mdahalo wa kitaifa wa vijana  kutoa mapendekezo kwa Rais Samia Suluhu Hassan. Mdahalo huo utajadili masuala kadhaa ikiwemo utekelezaji wa ajenda za kundi hilo, ikiwa ni sehemu ya kuangalia utendaji katika miaka mitatu ya Rais Samia madarakani na mwelekeo…

Read More

Tanzania, Estonia kubadilishana uzoefu matumizi akili bandia (AI)

Serikali ya Tanzania inatarajia kunufaika kupitia ushirikiano na nchi ya Estonia katika masuala ya Tehama na Usalama Mtandao ikiwemo kubadilishana uzoefu kwenye masuala ya akili bandia (Al), teknolojia ya mifumo kuzungumza, usalama wa mitandao (cybersecurity), namba ya utambulisho ya kidijitali, ubalozi wa data, uhuru wa data, ukuaji wa biashara changa na uchumi wa kidijitali. Kufuatia mazungumzo…

Read More

Mungai ashinda uenyekiti Chadema Iringa

Iringa. Mwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Iringa, William Mungai ameshinda nafasi hiyo kwa mara nyingine. Mungai ameshinda nafasi hiyo baada ya kuzoa kura 45 dhidi ya kura 34 ambazo mpinzani wake, Emmanuel Chengule amepata. Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi huo John Mrema amesema kila mgombea alipata haki ya kujieleza na kuchaguliwa. Katika…

Read More

Uchaguzi Chadema Njombe wavurugika tena

Dar es Salaam. Uchaguzi wa kumpata mwenyekiti wa Mkoa wa Njombe, uliowakutanisha Rose Mayemba na Ahadi Tweve umevunjika baada ya kutokea ugomvi baina ya pande mbili zinazowaunga mkono wagombea hao. Uchaguzi huo umevunjika leo Ijumaa Mei 24,2024 baada ya kutokea sintofahamu iliyosababishwa na wanachama waliodai kuwa kuna baadhi ya wajumbe kutoka Wilayani Makete hawakupaswa kushiriki…

Read More

Wabunge wacharuka migogoro ya ardhi, fidia kwa wananchi

Dodoma. Wabunge wamecharuka kuhusu migogoro ya ardhi na ucheleweshaji wa fidia kwa wananchi wanaopisha maeneo kwa ajili ya miradi. Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara ametaja vifo na majeruhi waliotokana na fidia isiyo na masilahi kwa wananchi wanaopisha maeneo ya uchimbaji. Wabunge wameeleza hayo wakichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba…

Read More

JKT laita vijana waliomaliza kidato cha sita kambini

Dodoma. Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limewataka wazazi wa vijana wanaoitwa kujiunga na mafunzo kwa mujibu wa sheria mwaka 2024 wasikubali kutapeliwa kwa kutozwa fedha. Vijana waliomaliza kidato cha sita mwaka huu, wametakiwa kuripoti katika kambi za JKT kuanzia Juni Mosi hadi 7, 2024. Akizungumza leo Mei 24, 2024, Mkuu wa Tawi la Utawala wa…

Read More

RC Mbeya atoa neno wafanyabiashara waliogoma Soko la Mwanjelwa

Mbeya. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amewataka wafanyabiashara mkoani humo, kuachana na migomo kabla ya kufanya mazungumzo na viongozi wa mamlaka. Amesema kufanya hivyo ni kutaka kuichafua  Serikali. Kauli hiyo ya Homera inakuja ikiwa ni siku moja  tangu wafanyabiashara wa maduka katika soko la Mwanjelwa kugoma kufungua maduka yao, wakidai kunyanyaswa na Mamlaka…

Read More

T: Sh10.5 bilioni kupiga jeki ajira sekta ya uvuvi

Mwanza. Ili kukabiliana na changamoto ya ajira nchini, Serikali kupitia Wizara ya Uvuvi na Mifugo, imetenga Sh10.5 bilioni kwa ajili ya kuwezesha mitaji na miradi ya vijana. Kauli hiyo imetolewa leo Mei 24, 2024 na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi kwenye hafla ya kufunga mafunzo kwa…

Read More