
Mafundi sanifu wataka kada hiyo kutambulika kielimu
Dodoma. Mafundi sanifu nchini wameiomba Serikali kuitambua kada hiyo kwenye ngazi ya shahada za uzamili na uzamivu wakieleza wanalazimika kubadilisha fani kwenda kwenye uhandisi ili kujiendeleza kielimu. Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Menye Manga leo Alhamisi Mei 23, 2024 kwenye mkutano mkuu wa sita wa mafundi sanifu nchini…