
Rais Samia muonee huruma Dk. Phissoo
RAIS wangu mama Samia, wiki iliyopita baada ya kuwa nimekuandikia kuhusu upandaji holela wa bei za mafuta ya nishati, mwana mwema mmoja kati ya wengi walioniandikia, alisema; “kwema ndugu mwandishi? Binafsi nakuombea Mungu akulinde na akutete dhidi ya watesi wenye lengo la kuihujumu kalamu yako, maana nijuavyo haya uyaandikayo hawayapendi. Wanapenda tuendelee kuwa mbumbumbu ili…