
Dereva bodaboda, mwenzake jela kwa kuiba kilo 120 za korosho
Dar es Salaam. Dereva bodaboda, Mbwana Kamote (30) na mfanyabiashara Nyatko Ngusi (47) wamehukumiwa kifungo cha miezi sita jela, baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa kilo 120 za korosho, zenye thamani ya Sh2.1milioni. Kamote na Ngusi, wamehukumiwa kifungo hicho, katika Mahakama ya Mwanzo Kariakoo, jijini Dar es Salaam jana Jumatano, Mei 22, 2024…