
Israel yafanya mashambulizi Kaskazini na Kusini mwa Gaza – DW – 21.05.2024
Katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia jeshi la Israel lilitumia matingatinga kuyasambaratisha maduka na majengo mengine karibu na soko katika operesheni inayoendelea iliyoanza wiki mbili zilizopita. Israel inadai kuwa imerejea kwenye kambi hiyo ambako miezi miwili iliyopita ilidai kuwa ililisambaratisha kundi la Hamas. Hayo yakijiri Wizara ya afya ya Palestina imeripoti kuwa vikosi vya Israel…