MSOMERA WANAPIKA KISASA – Mzalendo

Upishi wa kutumia kuni na mkaa kwa wakazi wa kijiji cha Msomera, wilayani Handeni Mkoa wa Tanga unakuwa ni historia mara baada ya wakazi hao kupatiwa majiko banifu na mitungi ya gesi ya kupikia. Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi majiko hayo katika Kijiji hicho jana Mei 17, Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema…

Read More

Meridianbet watoa msaada wa chakula Chamazi

  JUMAMOSI ya leo Meridianbet wametua pale Chamazi Magengeni kwaajili ya kutoa msaada wa vyakula kwa wakazi wa hapo hasa kwa zile familia ambazo zina uhitaji na zisizjiweza kwa kushirikiana na KMC. Meridianbet ambao ndio wadhamini wakuu wa KMC, timu ambayo msimu huu imekuwa na mwenendo mzuri kwenye ligi ikishika nafasi ya 5 mpaka sasa…

Read More

Watu wenye ulemavu wadai waajiri hawafuati Sheria ya Ajira

Mwanza. Watu wenye ulemavu wamelalamikia ukiukwaji wa Sheria ya Ajira inayoelekeza kampuni na mashirika kuajiri angalau wafanyakazi watatu wenye ulemavu kati ya 20 kuwa haizingatiwi. Pia, wamelalamikia ushirikishwaji mdogo kwenye fursa za kimaendeleo zinazotolewa na Serikali na wadau wa maaendeleo pamoja kukithiri kwa baadhi ya vitendo vya ubaguzi. Wakizungumza leo Jumamosi Mei 18, 2024 kwenye…

Read More

Sido yaja na mwarobaini kukabili sumu kuvu

Lindi. Vijana zaidi ya 50 wamepatiwa mafunzo ya utengenezaji wa vihenge ili kukabiliana na sumu kuvu. Mafunzo hayo yametolewa na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (Sido)Mkoa wa Lindi. Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumamosi Mei18,2024 wakati wa kufunga mafunzo  hayo, Mratibu wa Kuendeleza Teknolojia,  Mhandisi Abraham Malay amesema mafunzo hayo yamelenga  kuwasaidia vijana kukabiliana na…

Read More

Faru waliotoweka kwa miaka 30 kurejeshwa Hifadhi ya Mikumi

Morogoro. Baada ya faru weusi kutoweka kwa zaidi ya miaka 30 iliyopita kutokana na kuuawa na majangili, Serikali kupitia Hifadhi za Taifa (Tanapa), imeanza mchakato wa kuwarejesha katika Hifadhi ya Mikumi. Faru weusi wako kwenye orodha ya wanyama walio hatarini kutoweka duniani huku Tanzania kupitia mpango wa Taifa wa miaka mitano wa uhifadhi wa faru…

Read More

Majaliwa kuongoza kongamano wanahabari mitandao ya kijamii

Na Nora Damian, Mtanzania Digital Zaidi ya washiriki 500 wanatarajia kushiriki katika kongamano la wanahabari wa mitandao ya kijamii litakalofunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Kongamano hilo lililoandaliwa kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Mitandao ya Kijamii Tanzania (Jumikita) na Shirikisho la Serikali za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania (Tahliso) litafanyika Mei 20,2024 jijini Dar es…

Read More

Wakazi Handeni wataka bei rafiki gesi ya kupikia

Tanga. Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga, wameishauri Serikali kuangalia uwezekano wa kuweka bei rafiki ya kubadilisha mitungi ya gesi ya kupikia itakayosaidia hata wenye kipato kidogo kuimudu. Wakizungumza kwenye hafla ya kugawa majiko banifu na mitungi ya gesi kwa wananchi wa eneo hilo iliyofadhiliwa na Serikali kupitia Wakala wa Nishati…

Read More